ALESELEMA!
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefunguka kuwa
kutoonekana kwake kwenye ushabiki wa vyama na wagombea kama wasanii
wengine si kwamba hana ushabiki lakini moyoni mwake yupo Team ya Dk.
John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kajala
aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa pamoja na mbwembwe za watu kujiweka
wazi kuhusu chama na wagombea wanaowakubali, yeye mambo yake ni
kimyakimya kama alivyo mgombea wake wa urais kupitia chama hicho.
“Nimekuwa
kimya kwa muda mrefu kwa sababu hata mgombea wangu wa urais, Magufuli
ni mtu wa kimyakimya ila mtendaji mzuri, ndiye anastahili kura yangu,”
alisema Kajala.
Source:Global Publishers
Source:Global Publishers
No comments:
Post a Comment