KIMENUKA! Baada ya madai kwamba mtoto Latifah ‘Tiffah’ si damu ya Mbongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku shemeji wa zamani wa Zarinah Hassan
‘Zari’ (mama Tiffah), King Lawrence naye kusema mtoto huyo ni wake, kuna
taarifa mpya zinazodai kuwa, Zari ameitwa kwao, Uganda ili akamalize
ubishi juu ya suala hilo, Risasi Jumamosi limenasa mchapo kamili.
Hivi karibuni baada ya Zari kujifungua, King Lawrence alijitokeza na
kudai kuwa, mtoto huyo ni wake na kusema kama kuna anayebisha kiitishwe
kipimo cha vinasaba (DNA), hivyo kuibua mkanganyiko na taarifa
zilizozagaa awali kuwa, mtoto huyo ni wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan
Ssemwanga.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni, Zari alipigiwa simu na mama
yake mzazi, Halima Hassan akimtaka aende nyumbani kwao ili akawaeleze
ukweli ndugu zake ambao wamekuwa njia panda baada ya kuibuka kwa taarifa
kwamba Tiffah si wa Diamond ambaye familia inamtambua kwa sasa.
“Taarifa zinawafikia tofauti. Kuna zile za awali kwamba mtoto huyo ni wa
Ivan, mara zikaibuka nyingine kwamba ni wa King Lawrence hivyo mama
amemuita Zari ili akategue kitendawili hicho kumaliza ubishi.
ATAKIWA KWENDA NA UKWELI
“Amemtaka aende na ukweli moyoni maana yeye (Zari) ndiye anayeujua. Hata
hiyo DNA haina maana. Ameambiwa kwamba siku zote mama ndiye anayejua
ukweli wa mtoto ni wa nani,” kilisema chanzo hicho.
ATAKIWA AMUOGOPE MUNGU
Chanzo kilizidi kunyetisha kuwa, mbali na kumtaka aende na ukweli,
familia imemtahadharisha atakapofika aseme ukweli kwa kumuogopa Mungu
maana vinginevyo dhambi hiyo itamhukumu maisha yake yote.
“Ametahadharishwa na familia kwamba anapaswa kumuogopa Mungu maana ni
dhambi mtoto wa baba huyu kumpa baba huyu. Wao Kama familia wanajua
Tiffah ni wa Diamond. Sasa wanakangaywa na hao wanaodai wao ndiyo haswa
wahusika.
HAWAHOFII KAMA SI WA DIAMOND
“Familia imesema haina shida hata kama itakuwa mtoto si wa Diamond lakini wanachotaka wao ni kujua ukweli tu.” Chanzo.
DIAMOND ANASEMAJE?
Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu hivi karibuni baada ya King
Lawrence kuibuka na barua ya wakili kuitisha kipimo cha DNA akidai mtoto
ni wake, Diamond alisisitiza kwamba mtoto huyo ni damu yake hivyo hana
muda wa kubishana na mtu.
“Huyo jamaa (King Lawrence) atakuwa anatafuta kiki katika vyombo vya
habari. Huyohuyo ndiye alianza kusema mtoto si wangu ni wa Ivan mara
amegeuka tena na kusema ni wake yeye, hata haeleweki. Siwezi kujibishana
naye.
“Hata hiyo barua aliyosema ni ya wakili ya kutaka DNA, haijatufikia!
Nasikia tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” alisema
Diamond.
KUHUSU SAFARI
Alipotafutwa Diamond ili aeleze kuhusu taarifa za mama Tiffah kuitwa
nchini Uganda ili akaeleze ukweli, alisema hayo ni mambo ya kifamilia
zaidi na hata hivyo haoni tatizo ndugu kumwita Zari kwani ukweli Tiffah
ni damu yake na hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea.
“Tiffah ni damu yangu hata akienda hakuna kitakachobadilika. Sina
wasiwasi maana mimi najua mahesabu yake yote na ninajua mpaka tarehe
niliyokutana naye na mtoto akawepo,” alisema Diamond huku akisema, Zari
hana nafasi ya kuongea na vyombo vya habari.
NCHINI UGANDA
Nchini Uganda, bado baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti
mkanganyiko wa mtoto wa Diamond ambapo baadhi ya magazeti yametaka Zari
aende akapime DNA ili kujiridhisha kuhusu uhalisia.
AFRIKA KUSINI
Nazo habari kutoka nchini Afrika Kusini ambako ndiko kwenye makazi ya
Zari, baadhi ya Wabongo wanaoishi jirani na Zari walisema wanatambua
uwepo wa Diamond kama mpenzi mpya wa Zari kwa hiyo hakuna shaka kuwa
yeye ndiye baba (biological father) wa Tiffah.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu juzi, mkazi mmoja wa
eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Steve, alisema amekuwa
akimfuatilia kwa karibu King Lawrence kupitia Instagram yake akidai
kwamba yeye ni baba wa Tiffah, lakini sehemu kubwa ya watu wenye ujirani
na Zari kule wanaamini, Diamond ndiye baba husika.
“Kuhusu Diamond kuwa baba wa Latifah hilo halina ubishi. Hata sisi huku
tunajua hivyo. Hili suala liangaliwe kwa macho matatu. Nahisi kuna
‘vita’ ya sisi Watanzania na Waganda kuhusu mtoto,” alisema Mbongo huyo.
Source:Globalpublishers
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment