KIMENUKA! Baada ya madai kwamba mtoto Latifah ‘Tiffah’ si damu ya Mbongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku shemeji wa zamani wa Zarinah Hassan
‘Zari’ (mama Tiffah), King Lawrence naye kusema mtoto huyo ni wake, kuna
taarifa mpya zinazodai kuwa, Zari ameitwa kwao, Uganda ili akamalize
ubishi juu ya suala hilo, Risasi Jumamosi limenasa mchapo kamili.
Hivi karibuni baada ya Zari kujifungua, King Lawrence alijitokeza na
kudai kuwa, mtoto huyo ni wake na kusema kama kuna anayebisha kiitishwe
kipimo cha vinasaba (DNA), hivyo kuibua mkanganyiko na taarifa
zilizozagaa awali kuwa, mtoto huyo ni wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan
Ssemwanga.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni, Zari alipigiwa simu na mama
yake mzazi, Halima Hassan akimtaka aende nyumbani kwao ili akawaeleze
ukweli ndugu zake ambao wamekuwa njia panda baada ya kuibuka kwa taarifa
kwamba Tiffah si wa Diamond ambaye familia inamtambua kwa sasa.
“Taarifa zinawafikia tofauti. Kuna zile za awali kwamba mtoto huyo ni wa
Ivan, mara zikaibuka nyingine kwamba ni wa King Lawrence hivyo mama
amemuita Zari ili akategue kitendawili hicho kumaliza ubishi.
ATAKIWA KWENDA NA UKWELI
“Amemtaka aende na ukweli moyoni maana yeye (Zari) ndiye anayeujua. Hata
hiyo DNA haina maana. Ameambiwa kwamba siku zote mama ndiye anayejua
ukweli wa mtoto ni wa nani,” kilisema chanzo hicho.